11 Oktoba 2026 - 21:54
Ofisi ya Ayatullah Sistani: Jumanne Itakuwa Siku ya Kwanza ya Mwezi wa Jumada al-Ula

Ofisi ya Ayatullah Sistani imetangaza kuwa Jumanne, tarehe 13 Oktoba 2026, itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Jumada al-Ula, mwaka 1448 Hijria.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Ofisi ya Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali al-Husseini Sistani, Marjaa Mkuu wa Waislamu wa Kishia, imetangaza kuwa Jumanne, tarehe 13 Oktoba, sawa na tarehe 21 Mehr kwa kalenda ya Kiirani, itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Jumada al-Ula, mwaka 1448 Hijria.

Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Iraq (WAA), Ofisi ya Ayatullah Sistani ilitangaza katika taarifa iliyotolewa Jumapili kwamba Jumatatu itakuwa siku ya kukamilisha mwezi wa Rabiul-Thani, huku Jumanne ikiwa siku ya kwanza ya mwezi wa Jumada al-Ula.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha